Utalii: Wadau walalamikia kuongezwa kwa ushuru Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Utalii: Wadau walalamikia kuongezwa kwa ushuru Tanzania

Watalii nchini Tanzania hivi sasa wanalipa gharama zaidi katika malazi na gharama zingine za kuingia mbugani baada ya ushuru mpya wa VAT kuwekwa. Tanzania inasema asilimia 18 ya ushuru huo wa VAT inahitajika kuiongezea serikali mapato. Utalii unachangia takribani asilimia 14 ya uchumi wa nchi hiyo. Lakini wadau wengi wa utalii wamemwambia Mwandishi wetu Sammy Awami kwamba ushuru huo una madhara katika sekta ya utalii na kwamba biashara zao zimeathirika.