Kizza Besigye azungumza kuhusu uchaguzi Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Kizza Besigye azungumza kuhusu uchaguzi Uganda

Ni mtu aliyetawala siasa za upinzani Uganda kwa zaidi ya miongo minne sasa. Kizza Besigye. Amechuana na Rais Museveni kwenye uchaguzi mara tano! Uchaguzi wa Februari mwaka huu uliompa ushindi Rais Museveni, Besigye anasisitiza kuwa alishinda. Amediriki kujitangazia kuwa Rais wa Uganda na akaingia matatani. Sasa anakabiliwa na kesi ya Uhaini na yuko nje kwa dhamana. Amekuwa akizuru Marekani na Uingereza na kuzungumza na raia wa Uganda. Leo alitembelea studio zetu mjini London, na nilizungumza naye. Kwanza kujua tathmini yake ya uchaguzi wa mwaka huu.