Mapigano yazuka kumiliki visima vya mafuta nchini Libya

Badhi ya visima vya mafuta Libya
Image caption Badhi ya visima vya mafuta Libya

Mapigano mapya yameanza kuhusu mzozo wa umiliki wa baadhi ya visima vikubwa vya mafuta katika maeneo ya Mashariki nchini Libya.

Afisa mmoja wa usalama amekanusha kuwa vikosi vinavyomtii jenerali Khalifa Haftar vinadhibiti miji ya Sirda, Ras Lanuf na Zuitina.

Generali Haftar amekataa kutambua serikali ya umoja inayotambulika kimataifa huko Tripoli na kubaki upande wa watawala mahasimu wa Mashariki.