Paka aokolewa siku 16 baada ya tetemeko Italia

Paka aokolewa siku 16 baada ya tetemeko Italia

Paka mmoja ameokolewa kutoka kwenye vifusi siku 16 baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa mjini Amatrce, Italia.

Nyumba ya mmiliki wake iliporomoka kutokana na tetemeko hilo.

Paka huyo kwa jina Pietro kwa sasa anapokea matibabu katika kliniki ya daktari wa mifugo.

Iligunduliwa kwamba alikuwa amekwama kwenye vifusi baada ya wenye nyumba kurejea kujaribu kuokoa baadhi ya mali.

Watu karibu 300 walifariki kutokana na tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter.