Wachimba migodi wakwama chini ya ardhi Afrika Kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kuna maelfu ya wachimba migodi haramu nchini Afrika Kusini

Wachimba migodi haramu waliokuwa wamekwama chini ya ardhi kwenye mgodi mmoja nchini Afrika Kusini tangu siku ya Jumatano wameokolewa.

Polisi wanasema kuwa wanaume hao watatu walibuka kutoa ardhini mapema leo wakiwa wamejawa na vumbi, na kisha kutoroka wakihofia kukamatwa kwa kuendesha shughuli haramu.

Image caption Shughuli za uokoaji zinesitishwa kutokana na kuripotiwa kwa moto

Ripoti zaidi zinasema kuwa juhudi za uokoaji zimesitishwa kutokana na kuwepo moto chini ya ardhi, lakini jamaa za wachimba migodi waliokwama wanataka shughuli hiyo kuendelea.

Maelfu ya wachimba migodi wasio na vibali hufanya kazi kwenye migodi mingi ya dhahabu, maeneo yanayozunguka mji wa Johannesburg.