Mabaki ya MH370 yapatikana nchini Madagascar

Bwana Gibson anasema kuwa haijulikani ikiwa alama hizo zilisababishwa na moto kabla ya baada ya ajali Haki miliki ya picha BLAINE GIBSON
Image caption Bwana Gibson anasema kuwa haijulikani ikiwa alama hizo zilisababishwa na moto kabla ya baada ya ajali

Sehemu tano za mabaki ya ndege ambazo zinaweza kuwa za ndege iliyotoweka wa shirika la ndege la Malaysia ya MH370 zimepatikana nchini Madagascar.

Sehemu mbili zinaonekana kuonyesha alama ya kuchomeka ambazo ikiwa zitathibitishwa, itakuwa ndiyo mara ya kwanza alama kama hizo kupatikana.

Ndege ya MH370 iliyokuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing, ilikuwa na watu 239 wakati ilitoweka mwaka 2014.

Ndege hiyo inakisiwa kuanguka eneo la kusini mwa habari ya Hindi.

Sehemu hizo ziligunduliwa na mtafuta mabaki Blaine Gibson, ambaye awali amegundua mabaki mengine ya ndege hiyo.