Hichilema ashindwa kusimamisha kuapishwa kwa Lungu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hakainde Hichilema alipata asilimia 47.63 ya kura

Chama cha upinzani nchini Zambia cha United Party for National Development (UNDP) kimeshindwa katika jitihada zake kuzuia kuapishwa kwa rais hapo kesho.

Kiongozi wake Hakainde Hichilema alishindwa kwenye uchaguzi wa Agosti 11 na rais Edgar Lungu.

Lungu alipata asilimia 50.35 na kupita ailimia inayohitajika ili kuzuia kurudiwa kwa uchaguzi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Edgar Lungu alipata asilimia 50.35 ya kura

Akilalamikia udanganyifu, bwana Hichilema alienda katika mahakama ya kikatiba kutaka matokeo hayo kubatilishwa.

Lakini kesi hiyo ilikataliwa wakati majaji walisema kuwa chama cha UNDP hakikupeleka malalamiko yake kabla ya siku 14 ili kesi hiyo iweze kusikilizwa.

Hii leo chama hicho kilienda katika mahakama ya juu zaidi ambapo jaji alitoa uamuzi kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya kikatiba hauwezi kubatilishwa.