Wengi waishi kwa hofu ya madeni Zimbabwe

Watu wengi wamepoteza mali yao kwa wakusanya madeni au wanaishi kwa hofu ya nyumba zao kukabidhiwa wakopeshaji. Haki miliki ya picha Boldwell Hungwe
Image caption Watu wengi wamepoteza mali yao kwa wakusanya madeni au wanaishi kwa hofu ya nyumba zao kukabidhiwa wakopeshaji.

Wanawake nchini Zimbabwe wamepigwa picha wakishika barua za mwisho za kuwataka wafanye malipo wa madeni yao.

Zimbabwe kwa sasa inakumbwa na wimbi la watu walioshindwa kulipa madeni, wakati uchumi mbaya wa nchi hiyo unapoendelea kuwaathiri raia.

Wengi wamepoteza mali yao kwa wakusanya madeni au wanaishi kwa hofu ya nyumba zao kukabidhiwa wakopeshaji.

Mwandisi wa BBC alizungumza na Hazel Mhembere mwenye umri wa miaka 32 ambaye anaishia katika mji wa Chitungwiza na ambaye anapitia taabu za kila siku.

Anasema kuwa yeye pamoja na mmewe Tafadzwa Chingandu, walipoteza kazi mwaka uliopita na wote walikuwa wamechukua mikopo.

Kutokana na hilo sasa hawana uwezo wa kulipa mikopo yao.