Maoni yatolewa kuhusu ishara za wanariadha wa Ethiopia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanariadha hao uzalendo wao kwa waandamanaji wa Oromo nyumbani Ethiopia.

Watu wengi wametoa maoni kuhusu taarifa iliyoandikwa na BBC kuhusu mwanariadha wa mbio za walemavu Tamiru Demise, ambaye alifanya ishara ya X akitumia mikono juu ya kicha chake kama njia ya kupinga, wakati alipoelekea kumaliza mbio mjini Rio.

Alikuwa akionyesha uzalendo wake kwa waandamanaji wa Oromo nyumbani Ethiopia.

Ishara inajiri baada ya ile iliyofanywa na mwariadha mwenzake Feyisa Lilesa alipokuwa akikamilisha mbio zake katika mashindano ya olimpiki ya Rio.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Feyisa Lilesa

Feyisa sasa yuko Marekani na anasema kuwa hawezi kurejea nchini Ethiopia.

Wengi wameunga mkono hatua yake lakini wengine wanasema kuwa ni njama ya kutafuta hifadhi.