Sunderland kukipiga na Everton katika dimba la Light

Jermain Defoe Haki miliki ya picha Google
Image caption Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe

Ligi kuu ya England itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo Sunderland watawaalika Everton.

Sunderland ama Paka weusi watakua nyumbani katika dimba la Light kusaka ushindi katika msimu huu dhidi ya The Toffes Everton.

Wachezaji wapya waliosajili siku za mwisho za usajili Mika Domingues na Jason Denayer wanatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha David Moyes.

Mshambuliaji Victor Anichebe na Didier Ndong hawatakuepo kwenye mchezo huo huku Jan Kirchhoff, Jordan Pickford na John O'Shea wakiwafiti kwa mchezo.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Beki kisiki wa Everton Phil Jagielka

Mshambuliaji mpya wa Everton, Enner Valencia, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitachoanza mchezo huo. Beki wa kulia Seamus Coleman amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Everton baada ya kupona maumivu ya enka.

Pia viungo Darron Gibson na Tom Cleverley wanatarajiwa kuwa fiti kucheza, The Toffes watamkosa kiungo wao mahiri James McCarthy aliefanyiwa upasuaji.