Ajipata taabani kwa kuandika mzaha kwenye Facebook

#KenWaMwangi aliandika ujumbe unaohusu ngona na watoto kwenye ukurasa wake wa Facebook Haki miliki ya picha AFP
Image caption #KenWaMwangi aliandika ujumbe unaohusu ngona na watoto kwenye ukurasa wake wa Facebook

Mwanamme mmoja nchini Kenya amejikuta taabani baada ya kuandika ujumbe ambao alitarajia kuwa mzaha, kuhusu ngono na watoto katika ukurasa wake wa mtandao Facebook.

Ukurasa wake wa jina #KenWaMwangi umekuwa ukizungumziwa kwa saa kadha nchini Kenya huku watu wakimkosoa kwa yale aliyoyaandika.

Licha ya yeye kufuta ujumbe huo na kuomba msamaha, watu wamekuwa wakituma ujumbe huo ulionakiliwa mapema.

Mwajiri wake ambayo ni halmashuari la viwanja vya ndege nchini Kenya, inasema kuwa yale yaliyoandika yanaenda kinyume na sera zake na kwamba inafanya uchunguzi.