Familia za wahanga wa shambulizi la Septemba 11 kuishitaki Saudi Arabia

Rais Barack Obama
Image caption Rais Barack Obama

Ikulu ya marekani imesema kuwa Rais Obama atapitisha muswada kwa bunge mbili za Marekani kuruhusu familia za wahanga waliokufa kwenye shambulizi la septemba 11 kuishtaki Saudi Arabia.

Msemaji wa ikulu Josh Earnest amesema kuwa kama muswada huo utakua sheria basi kuna uwezekano mkubwa nchi nyingine zitalipisha raia wa Marekani.

Mapema kundi la nchi sita za kiarabu ikiwemo Saud Arabia walionesha hisia zao kuhusu suala hilo na kusema kuwa ni kinyume na kanuni za sheria ya kimataifa.

Image caption Miongoni mwa majina ya waliouawa katika shambulizi hilo

Wahalifu 15 kati ya 18 waliohusika katika mashambulizi ya huko New York na Pennsylvania ni raia wa Saud Arabia.