Kiongozi wa IS auawa kwa shambulizi za ndege za angani Syria

Abu Mohamed al-Adnan
Image caption Abu Mohamed al-Adnan

Pentagon imethibitisha kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi lenye itikadi kali la dola la kiislam Abu Mohamed al-Adnani ameuawa katika shambulizi la anga huko kaskazini mwa Syria mwezi uliopita.

Taarifa ya msemaji wake imeeleza kuwa ndege ya Marekani ilifanikiwa kumlenga na kumuua.

Kundi la dola la kiislam lilithibitisha kuwa amekufa, lakini Marekani na Urusi wote wanadai kuhusika na shambulio hilo.