Katika muendelezo wa makala za wiki hii,fahamu baadhi ya tamaduni zilizoanza kutoweka Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Fahamu baadhi ya tamaduni zilizoanza kutoweka Tanzania

Maeneo ya mwambao wa pwani nchini Tanzania,kama vile Tanga, kwa muda mrefu yamekuwa yakisifika kwa kudumisha utamaduni wa kiswahili hasa katika mavazi, vyakula na mengineyo.Lakini katika miaka ya hivi karibuni, utamaduni huo umepata changamoto ya kupotea haswa baada ya kuingia kwa utamaduni wa Kimagharibi.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau hivi karibuni alitembelea mkoa huo wa Tanga na kuangalia baadhi ya tamaduni hizo zinazopotea akianza na utamaduni wa mapambo ya makawa.