Maafisa watathmini athari za tetemeko Bukoba, Tanzania

Maafisa watathmini athari za tetemeko Bukoba, Tanzania

Rais wa Tanzania, John Magufuli, ameahirisha ziara yake ya kwenda nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu kufuatia tetemeko la ardhi kwa mikoa ya kanda ya ziwa hususan mkoa wa Kagera.

Mazishi yanaendelea kufanyika na majeruhi wanaendelea kupata nafuu, wakati tathimini ikiendelea kufanyika pia juu ya athari kamili za tetemeko hilo siku ya Jumamosi.

Tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 5.7 katika kipimo cha Richa, limeelezewa kuwa ndio lenye madhara zaidi kuwahi kutokea nchini humo, ambapo watu 16 walifariki dunia na wengine zaidi ya 250 kujeruhiwa.

Mwandishi wetu Sammy Awami yupo mjini Bukoba na ametutumia taarifa ifuatayo.