Bajaji isiyotumia mafuta yawasili Uingereza

Naveen Rabelli Haki miliki ya picha PA

Mhandisi kutoka India, ambaye amekuwa akiendesha bajaji ya kutumia kawi ya jua, amewasili Uingereza baada ya safari iliyodumu miezi saba.

6,200 mile (9,978km) journey.

Naveen Rabelli, 35, ambaye ni mzaliwa wa Australia, aliendesha bajaji yake kutoka kwenye feri Dover, Uingereza akiwa amechelewa kwa siku tano.

Alitarajia kufika mapema lakini akakwama kwa muda Paris baada ya pasipoti na kipochi chake kuibiwa.

Safari hiyo ni ya umbali wa kilomita 9,978.

Lengo lake Bw Rabelli katika kufanya ziara hiyo lilikuwa kuhamaisha watu kutumia magari yanayotumia kawi mbadala kama vile sola au umeme.

Anapanga kuhitimisha safari yake katika kasri la Buckingham, London.

Anasema amefurahia sana kwamba watu wamekuwa wakijitokeza kumsaidia na kumshangilia akiwa safarini.

"Watu hupenda bajaji hii. Hujitokeza na kupiga selfie. Ninapowaambia kwamba haitumii petroli, huwa wanashangaa sana."

Haki miliki ya picha PA

Alianzia safari yake Bangalore nchini India kisha akaendea Iran. Alipitia Uturuki, Bulgaria, Serbia, Austria,Uswizi, Ujerumani na Ufaransa

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii