Mhubiri anayepinga mapenzi ya jinsia moja azuiwa kuingia Afrika Kusini

Image caption Steve Anderson anapinga mapenzi ya jinsia moja

Afrika Kusini imemzuia mhubiri mmoja kutoka nchini Marekani kuingia nchini humo kutokana na matamshi yake yanayopinga mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Afrika Kusini alisema kuwa Steven Anderson alinyimwa visa kwa sababu katiba hauruhusu kutolewa matamshi ya uchochezi.

Bwana Anderson anaongoza kanisa la Faithful Word Baptist, ambalo linasema kuwa mapenzi ya jinsia moja ni jambo lisilokubalika na kwamba adhabu yake inastahili kuwa kifo.

Image caption Waziri wa mashauri ya kigeni Malusi Gigaba anasema kuwa uamuzi wake unaambatana na katiba

Anderson anasema kwa uhuru wa dini haupo nchini Afrika Kusini.

Zaidi ya sahihi 60,000 zilizokusanywa na mashirika ya wapenzi wa jinsia moja na makundi ya wanaharakati nchini Afrika Kusini zilikuwa zimetoa wito wa kufutwa kwa safari hiyo.

Kanisa la bwana n Anderson lina makao yake katika jimbo la Arizona nchini Marekani.