Bosco Ntaganda agomea chakula mahakama ya ICC

Ntaganda analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ntaganda analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono

Kamanda wa zamani waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, ambaye anakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko Hague, amasema kuwa yuko tayari kufa badala ya kuvumilia hali anayopitia kwa sasa akiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la habari ya Reuters.

Bosco Ntaganda ambaye analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanawake kama watumwa wa ngono na pia mauaji nchini Jamhuri ya Demokrasia Congo kati ya mwaka 2002 na 2003, alianza mgomo wa kutokula chakula wiki iliyopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ntaganda anasema hana uwezo wa kumuona mkewe na watoto

"Sina uwezo wa kumuona mke wangu na watoto tena katika hali nilivyo sasa. Hii ndiyo sababu imenifanya nipoteze matumani.Ndiyo sababu niko tayari kufa," Ntaganda alisema katika taarifa iliyosomwa na wakili wake.

Ntaganda alikana mashtaka yote 18 dhidi yake wakati wa kuanza kwa kesi mwaka uliopita.