Islamic State wadai kuendesha shambulizi Mombasa

Image caption Wanawake hao waliwashambulia polisi wa visu

Taarifa moja kutoka kutoka kundi linalojiita Islamic State, inasema kuwa wanawake watatu waliouawa wakati walijaribu kushambulia kituo kikuu cha polisi katika mji wa pwani ya Kenya wa Mombasa siku ya Jumapili, walikuwa ni wafuasi wa Islamic State.

Wanawake hao waliokuwa wamevaa hijab waliingia katika kituo hicho wakisema kuwa walitaka kuandikisha taarifa kuhusu simu iliyokuwa imepotea kabla ya kuendesha shambulizi la kisu na bomu la petroli.

Taarifa iliyoandikwa katika mtandao wa simu wa Telegram, ilidai kuwa kundi hilo ndilo lilihusika bila ya kutoka taarifa zaidi.

Pia kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa zinazodai kuwa kuna barua ambayo inakisiwa kuandikwa na wanawke hao ambapo wanatangaza kulitii kundi la Islamic State.