Kiongozi wa waasi wa FARC arejea nchini Colombia

Timochenko anahusishwa na mauaji mengi akiwa na kundi la FARC
Image caption Timochenko anahusishwa na mauaji mengi akiwa na kundi la FARC

Kiongozi wa waasi wa kundi la FARC, Rodrigo Londono, anaejulikana zaidi kwa jina la Timochenko, amerejea Colombia kutafuta idhini kwa kundi lake kwa ajili ya mkataba wa amani aliosaini na serikali mwezi uliopita.

Timochenko alisafiri kwa ndege binafsi kutoka Havana ambako makubaliano ya kutafuta amani yanafanyika.

Akiambatana na waliokuwa wapiganaji wa kundi, wakiwa njiani kuelekea kambi iliyopo kusini mwa nchi hiyo,ambapo mamia ya waasi wa kundi la FARC hukutana mwishoni mwa wiki.

Image caption Mamia ya waasi wa kundi la FARC hukutana mwishoni mwa wiki

Aidha Timechenko ameweamuru kundi la FARC kufanya vitendo vya umwagaji damu na mauwaji, ikiwemo kuteka nyara na kuua ikiwa ni pamoja na kutoa mchango muhimu katika kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya