Clinton kurejelea kampeni za uchaguzi Marekani

Hillary Clinton alipokuwa anawasili kwa sherehe za kukumbuka shambulio la 9/11 Haki miliki ya picha AP
Image caption Hillary Clinton alipokuwa anawasili kwa sherehe za kukumbuka shambulio la 9/11

Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton atarejelea kampeni zake mnamo Alhamisi, msemaji wake amesema.

Mwanasiasa huyo alikuwa amepumzika kwa siku kadha ili kupata nafuu baada ya kuugua kichomi.

Bi Clinton alizidiwa na nusura azirai alipokuwa anahudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 15 tangu kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi la 9/11 ambapo watu karibu 3,000 waliuawa.

Aligunduliwa kuwa anaugua kichomi, ugonjwa wa mapafu ambao pia hujulikana kama nimonia, siku ya Ijumaa.

Kumezuka mjadala mkali kuhusu afya yake Marekani, na muda ambao alichukua kupata nafuu, huku uchaguzi mkuu ukiendelea kukaribia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii