Ceferin achaguliwa kuwa Rais mpya wa Uefa

Alexander Ceferin Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alexander Ceferin Rais mpya wa Uefa

Rais wa chama cha soka cha Slovenia Alexander Ceferin amechaguliwa kuwa Rais mpya wa shirikisho la soka barani ulaya (UEFA)

Ceferin anachukua nafasi iliyowachwa wazi na Michel Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na kosa la kupokea mlungula wa £1.3mil.

Rais huyu mpya amemshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira cha Uholanzi katika kura iliyopigwa Leo jijini Athens.

Ceferin atashika kiti hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019