Collin Powell: Trump ni ''aibu kwa taifa''

Jenerali mstaafu Collin Powell
Image caption Jenerali mstaafu Collin Powell

Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Collin Powell ameripotiwa akimuita mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani kuwa ''aibu kwa taifa'',kulingana na barua pepe iliofichuliwa.

Matamshi hayo ya jenerali huyo aliyestaafu yalifichuliwa baada ya udukuzi wa barua pepe yake ya kibinafsi.

Barua hizo zilichapishwa katika mtandao wa DCLeaks.com,ambao pia umehusishwa na udukuzi mwengine wa viongozi wa ngazi za juu.

Bwana Powell,ambaye amenyamaza wakati wa uchaguzi alisema kuwa hana matamshi ya kuongezea lakini ''hakukataa madai ya barua hizo''.

Image caption Donald Trump

Pia alimkosoa mgombea wa chama cha Democrat vile alivyoangazia mzozo wake wa swala la barua pepe za kibinafsi.

Matamshi hayo kuhusu Trump ni miongoni mwa barua iliotumwa tarehe 17 mwezi Juni kwa Emily Miller,mwandishi na msaidizi wa zamani wa bwana Powell.