Mbuga kuua wanyama Afrika Kusini, majirani kupewa nyama

Baadhi ya Viboko watakaouliwa wakiwa katika Mbuga ya Wanyama ya Kruger nchini Afrika Kusini.
Image caption Baadhi ya Viboko watakaouliwa wakiwa katika Mbuga ya Wanyama ya Kruger nchini Afrika Kusini.

Wasimamizi wa mbuga kubwa zaidi ya wanyama wa pori nchini Afrika Kusini wameanza kupunguza wanyama kwa kuwaua na kutoa nyama yao kwa jamii zinazopakana na hifadhi hiyo.

Kulingana na shirika la habari la Associated Press hifadhi hiyo itawaua viboko na nyati 350.

Kulingana na takwimu za shirika la wanyama wa pori, Mbuga ya Kruger ina karibu viboko 7,500 na nyati 47,000.

Msemaji wa shirika la wanyama wa pori, Ike Phaahla, alisema kuwa wanyama hao wawili hula kiwango kikubwa cha mimea na kuwa kiangazi kinachotarajiwa kitasababisha vifo vingi vya wanyama, kulingana na AP.