Gazeti la Nation Mirror lililoandika makala ya rushwa lafungiwa Sudan Kusini

Rais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu wanashutumiwa kujilimbikizia mali wakati raia wakiteseka na vita
Image caption Rais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu wanashutumiwa kujilimbikizia mali wakati raia wakiteseka na vita

Mhariri wa gazeti linaloongoza Sudani Kusini amesema serikali imeamuru kufungwa kwa gazeti hilo, siku moja baada ya kuchapisha makala ya madai ya rushwa kwa maafisa wa ngazi za juu.

Siku ya jumanne gazeti la Nation Mirror lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari kuhusu ripoti ya waangalizi wa Marekani ambayo inamshtumu Rais Salva Kiir na viongozi wengine wa ngazi za juu kujilimbikizia mali wakati raia wa kawaida Sudan kusini wakihaha na hali mbaya ya maisha.

Mhariri wa gazeti hilo Aurelious Simon Chopee amesema kuwa hakuna taarifa yoyote rasmi aliyopewa juu ya kufungwa kwa gazeti hilo.

Na hakuna taarifa yoyote ile kutoka mamlaka ya nchi.

Serikali ya Sudan Kusini imekuwa ikikosolewa kwa kuwaekea vikwazo waandishi wa habari.