Mashirika ya haki za kibinaadam yamtaka Obama kumsamehe Snowden

Edward Snowden alivujisha taarifa za siri za Marekani miaka mitatu iliyopita
Image caption Edward Snowden alivujisha taarifa za siri za Marekani miaka mitatu iliyopita

Mashirika makuu matatu ya haki za binaadam yamemtaka Rais Barack Obama kumsamehe Marekani Edward Snowden.

Snowden ambaye alikuwa mchambuzi wa masuala ya kijasusi wa Marekani ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni mjini Moscow anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha kiwango kikubwa cha taarifa za siri miaka mitatu iliyopita.

Akihutubia mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya video akiwa Urusi, ameshukuru shirika la haki za binaadam la marekani, shirika la haki za binaadam la kimataifa, na shirika la kutetea haki za binaadam kwa kuanzisha kampeni za kusamehewa.

Alisema watu lazima wawe tiyari kufichua maovu ya serikali katika kulinda misingi ya demokrasia.