Hillary Clinton atoa maelezo zaidi kuhusu afya yake

Clinton anatarajiwa kurejelea kampeni Alhamisi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Clinton anatarajiwa kurejelea kampeni Alhamisi

Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic, nchini Marekani, Bi Hillary Clinton, ametoa maelezo zaidi kuhusu jinsi alivyougua ugonjwa wa kichomi.

Taarifa kutoka kwa makao makuu ya kampeni yake, imesema kuwa, Bi Clinton, anaugua ugonjwa wa kichomi ambao hauwezi kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Wakati huo huo mgombea wa chama cha republican, Donald Trump, amekiambia kituo kimoja cha runinga kuwa uchunguzi wa madaktari wa hivi karibuni ulibainisha kuwa ameongeza uzani wake ila yuko buheri wa afya.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii