Lowassa: Kuna dalili za ‘udikteta’ Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Lowassa: Kuna dalili za ‘udikteta’ serikali ya Magufuli Tanzania

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Edward Lowassa ameeleza wasiwasi wake kuhusu kile anachokitaja kama dalili za udikteta kwenye uongozi wa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Amesema hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya kuanzisha kampeni ya Ukuta.

Bw Lowassa aliwania urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka jana kwa tiketi ya chama cha Chadema lakini akashindwa na Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Mwandishi wa BBC John Nene amezungumza na Bw Lowassa mjini Nairobi, na anaanza kwa kuzungumzia uongozi wa Bw Magufuli.