Donald Trump asema uzani wake umezidi kiwango

Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump amesema anapokea matibabu kupunguza chorestrol

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema baadaye wiki hii atatoa ripoti ya kina kuhusu hali yake kimwili na kiafya.

Hata hivyo, amedokeza kwamba baada ya kupimwa, imebainika kwamba uzani wake umezidi kiwango na anahitaji kupunguza.

Mgombea huyo alitoa muhtasari wa hali yake kiafya kwenye karatasi ya ukurasa mmoja alipokuwa akishiriki katika kipindi cha televisheni cha The Dr Oz Show.

Alimwambia mtangazaji kwamba uzani wake ni 236lb (kilo 107.048) na kimo chake ni 6ft 3in, jambo linalomfanya kuwa na uzito kupita kiasi.

Amesema anatumia dawa za kupunguza kiwango cha cholesterol kwenye mwili wake, lakini yuko buheri wa afya.

Anadaiwa pia kuwa na viwango vya juu kuliko kawaida vya homoni za testosterone.

Makala kamili ya mahojiano yake ya mtangazaji huyo itapeperushwa hewani baadaye Alhamisi.

Maafisa wake wa kampeni wamesita kufichua yaliyomo kwenye uchunguzi huo.

Haki miliki ya picha AFP

Bw Trump aliambia mkutano wa siasa mjini Canton, Ohio, Jumatano usiku kwamba ana shaka kuhusu iwapo Bi Clinton, aliyezidiwa na kichomi Jumapili na kulazimika kuahirisha mikutano ya kampeni, ana uwezo wa kuongoza moja ya hafla zake.

Aliuliza umati: "Mnafikiri Hillary angeweza kusimama hapa kwa saa moja na kufanya hivi? Sidhani, sidhani anaweza."

Bw Trump baadaye alisema mgombea huyo wa chama cha Democratic "analala kitandani, akiendelea kupata nafuu".

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii