Kinywaji cha ''kupoteza ubikira'' chazua mjadala China

Kinywaji cha Four Loco chazua mjadala mkali nchini China Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Kinywaji cha Four Loco chazua mjadala mkali nchini China

Kinywaji maarufu kwa jina ''blackout in a can' nchini Marekani kimeingia nchini China.

Four Loko ,kinywaji kilicho na ladha ya matunda na asilimia 12 ya pombe kilitumika sana katika sherehe nchini Marekani kabla ya kuondolewa madukani katika majimbo kadhaa hadi pale viungo vyake viliporekebishwa.

Na sasa kimepata umaarufu mkubwa nchini China ,huku raia wakikiita ''Lose Virginity'' {poteza ubikira}kwa kuwa wanahisi kinywaji hicho kina nguvu zaidi.

Image caption Raia wengi wamekuwa wakijipiga picha wakinywa kinywaji hicho

Wanavlogu kadhaa wamepakia kanda za video wakinywa kinywaji hicho cha mililita 695.

Kinywaji hicho kiligonga vichwa vya habari hivi majuzi baada ya wanawake watatu walio katika umri wa miaka 20 kuficha na kuingiza kinywaji hicho katika baa moja ya karaoke,kupoteza fahamu baada ya kunywa na kupoteza vitu vyao vyote kwa wezi..

  • Je, Four Loko ni nini haswa ,na watu wanasema nini kuhusu kinywaji hiki?

Four Loko kimeelezewa katika mitandao ya kijamii nchini China kuwa kinywaji kilicho na pombe pamoja na kafeini.

Image caption Kinywaji cha Four Loco

Baadhi ya watu wanadai kwamba mchanganyiko huo unakifanya kinywaji hicho kuwa na nguvu na kina uwezo wa kumfanya mtu kupoteza fahamu baada ya kunywa chupa moja tu