Msongo wa mawazo watatiza wanajeshi wa zamani Kenya

Msongo wa mawazo watatiza wanajeshi wa zamani Kenya

Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa akili unaoweza kumuathiri mtu baada ya kushuhudia matukio ya kugutusha kama vita, ambayo humfanya mtu kuishia kutumia vileo, kujihusisha na ghasia au hata pia kujitoa uhai.

Wanajeshi wa Kenya, wamekuwa katika maeneo yanayokumbwa na mizozo kama Somalia. Kumeendelea kuwa na shutuma kutoka kwa walio ndani ya jeshi na wengine nje, kwamba hakuna usaidizi wa kutosha kwa walioathiriwa kiakili kutokana na wanayoyashuhudia katika maeneo hayo ya mizozo.

Sasa makundi tofuati ya umma, yameamua kuchukua hatua na kutoa usaidizi na uhamasisho kwa waathiriwa hao.

Maryam Dodo Abdalla anaarifu zaidi.