Baibui la ukaya, vazi la pwani linalosahauliwa
Huwezi kusikiliza tena

Baibui la ukaya, vazi la pwani linalosahauliwa

Baibui la ukaya katika mwanzoni mwa miaka ya hamsini hadi kufikia mwishoni mwa miaka ya themanini lilikuwa ni vazi muhimu kwa wanawake wa maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki.

Hii ni kutokana na uwezo wake wa kuhifadhi sehemu kubwa ya mwili wa mwanamke, hali inayoendana na itikadi za wanawake wa maeneo hayo.

Hata hivyo, hali hivi sasa imekuwa tofauti baada ya kuingia kwa mabaibui ya kisasa maarufu kama habaya hivyo kulifanya baibui la ukaya kuonekana kama limepitwa na wakati.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau alipotembelea mjini Tanga, alidadisi kwa nini hali imekuwa hivyo.