Ban Ki-moon akosoa pendekezo la Netanyahu kuhusu upanuzi wa makazi ya Israel

Upanuzi huo ni kinyume na sheria za umoja wa mataifa
Image caption Upanuzi huo ni kinyume na sheria za umoja wa mataifa

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amemkosoa vikali waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa pendekezo lake kwa wale wanaopinga upanuzi wa makazi ya Israel kuwa wao ni wafuasi wa kikabila.

Ban Ki-moon amesema kuwa maoni ya Netanyahu hayakubaliki na ni ya kichochezi.

Ban Ki-moon ambae anaondoka madarakani mwisho wa mwaka huu amewakumbusha Israel kuwa upanuzi huo wa makazi sio halali chini ya sheria ya kimataifa, na kwa lugha ya ukali Ban Ki-moon alisema Urusi lazima imalize ukandamizaji na uvamizi wa maeneo ya Palestina.