Chatu auawa kwenye shamba la Museveni

Haki miliki ya picha The Daily Monitor
Image caption Chatu aliyeuawa kwenye shamba la Museveni

Chatu mwenye urefu wa futi ishirini ameuawa kwenye shamba la Rais wa Uganda Yoweri Museveni eneo la Kisozi lililo wilaya ya Gomba.

Polisi walimuua kwa kumpiga risasi chatu huyo mara tatu, alipojaribu kungia shamba hilo ambapo rais Museveni anafunga ng'ombe wengi.

Polisi mmoja anasema kuwa walishikwa na uoga walipomuona chatu huyo, ndipo wakaamua kumpiga risasi ili kuokoa ng'ombea wa rais.

Watu watatu walikamatwa wiki iliyopita kufuatia madai ya kumuibia Raisi museveni ng'ombe.

Rais Museveni hufuga ng'ome wenye pembe ndefu ambao kitamaduni hufugwa na watu wa kabila lake la Banyankore.

.