Tamasha za bia zaanza Ujerumani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tamasha za Oktoberfest huwavutia zaidi ya wageni milioni 6 kutoka kote duniani

Polisi nchini Ujerumani wamedumisha usalama wa hali ya juu wakati inapo anza tamasha kubwa ya bia duniani inayofahamika kama Oktoberfest ambayo inaanza leo mjini Munich.

Utawala unahofu kuwa tamasha hiyo inaweza kulengwa na magaidi kufuatia mashambulizi mabaya yaliyotokea msimu uliopita wa joto.

Kwa mara ya kwaza eneo la tamasha hilo la Oktoberfest litazungukaw na ua. Walinzi zaidi wamepelelekwa pamoja na kamera zaidi za usalama.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ulinzi mkali umedumishwa eneo la tamasha

Naibu Meya wa Munich amesema kuwa hatua hizo zilichukuliwa ii kujitahadharisha kufuatia visa vya hivi majuzi bila ya kubadilisha sura ya tamasha hizo.

Takriban wageni milioni 6 kutoka kote duniani wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hizo ambazo hufanyika kila mwaka.