Sudan Kusini yakanusha madai ya ufisadi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Viongozi wa Sudan Kusini walilaumiwa kwa kujilimbikizia mali

Serikali ya Sudan Kusini imekanusha madai ya ufisadi yaliyotolewa kwenye ripoti ya shirika moja la Marekani kwamba madai hayo ya ufisadi miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu nchini humo wanayumbisha pia mchakato wa amani wa nchi hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza jinsi vigogo wanavyojilimbikizia mali huku wananchi wa kawaida wakiteseka kutokana na madhila ya vita.

Msemaji wa rais Salva Kiir, anasema madai hayo hayana msingi wowote na kuwa mataifa ya magharibi yanataka kuchochea mapinduzi ya serikali yake.