Marekani na Urusi watupiana lawama Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Putin awalaumu waasi kwa kujikusanya upya

Rais Vladimir Putin wa Urusi amewakashifu wale anaowaita vikosi vinavyopinga utawala wa Rais Assad kwamba wanajikusanya upya wakitumia fursa ya tangu juzi ya usitishwaji mapigano .

Bw Putin amemtetea rais Assad kwamba yeye anaheshimu mapatano hayo ya kusitisha mapigano lakini akalitaja kundi lililokuwa likijiita al-Nusra Front kama la kigaidi ambalo linachukua fusra hiyo kujipanga upya.

Wote Marekani na Urusi wanasema wangependa mda wa siku 4 wa kipindi walichoafikiana cha kusitisha mapigano huko Syria uongezwe.

Image caption Marekani inamtaka Assad aruhusu misaada kufika Allepo

Hata hivyo wamelaumiana kwa kutochukua juhudi zaidi kuhakikisha mkakati huo unafanya kazi kama inavyopaswa.

Urusi wanaitaka Marekani ishawishi makundi mbalimbali ya waasi waheshimu makubaliano hayo.

Nao Marekani wanaitaka Urusi iushawishi utawala wa rais Bashar al- Assad uruhusu misafara ya kutoa huduma za kibinadamu iwafikie waathiriwa wa vita huko mjini Aleppo.