Hali ya wasi wasi yashuhudiwa Kashmir India

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Polisi wanawafyatulia waandamanaji kokoto inayoweza kuua

Amri ya kutotoka nje imetolewa katika jimbo lote la Kashmir linalotawaliwa na India, baada ya maiti ya mvulana wa shule kupatikana katika barabara kuu ya mji wa Srinagar, ukiwa umejaa majaraha ya kokoto alizorushiwa.

Askari wa usalama wameendelea kufyatua kokoto hizo, ambazo zinaweza kuuwa.

Askari wanawafyatulia waandamanaji wanawanaotaka kuitenga Kashmir hata baada ya serikali kusema itatumia mbinu nyengine.

Image caption Vizuizi vimewekwa kwenye barabara inayoelekea mji wa Srinagar

Ripoti zinasema polisi walitumia moshi wa kutoza machozi dhidi ya maelfu ya watu waliohudhuria mazishi ya mtoto huyo.

Wakuu pia wamefunga huduma zote za mtandaoni.

Mwandishi wa BBC mjini Srinagar anasema, vizuizi hivyo ni vikali kabisa tangu maandamano dhidi ya India kuanza mwezi Julai.