Jeshi la Uingereza halina uwezo wa kuilinda nchi

Image caption General Sir Richard Barron

Imekuja kujulikana kuwa kamanda mmoja wa jeshi la Uingereza ameionya serikali kwamba vikosi vya jeshi la Uingereza havitoweza kuilinda nchi kukitokea shambulio kamili la kijeshi.

Jenerali Sir Richard Barrons, alieleza tathmini yake hiyo kali, kwenye barua aliyotuma kabla ya kustaafu kama kamanda (Joint Forces Command) mwezi wa Aprili.

Alisema uwezo wa jeshi umepunguzwa ili kupunguza gharama.

Haki miliki ya picha MOD
Image caption Uwezo wa jeshi umepunguzwa ili kupunguza gharama.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema bajeti ya jeshi inaongezeka, na kwamba uamuzi uliofikiwa uliungwa mkono na wakuu wa jeshi, pamoja na Sir Richard.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea