Ndege yaangukia nyumba,watu wote wanusurika Marekani

Ndege yaangukia nyumba nchini Marekani
Image caption Ndege yaangukia nyumba nchini Marekani

Rubani ,pamoja na warukaji wa 4 wa angani pamoja na wakaazi wawili wa nyumba wamenusurika kifo baada ya ndege moja kuanguka katika nyumba moja mjini Phoenix, Arizona.

Maafisa wa kukabiliana na moto katika makaazi ya Gilbert wanasema watu waliokuwepo katika ndege hiyo waliweza kutoka ndani ya ndege hiyo kabla ya kunagukia nyumba hiyo.

Kulikuwa na watu wawili ndani ya nyumba hiyo ,lakini hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa.

Rubani wa ndege hiyo alipelekwa hospitalini na kutibiwa majeraha madogo madogo ya moto kulingana na polisi.

Hakuna mrukaji wa angani aleyeumia .Inadaiwa kwamba ndege hiyo ilikuwa ikibeba warukaji wa angani kwa sherehe ya katiba,siku inayoadhimishwa kila mwaka kusherehekea katiba ya Marekani.