Boti illiojaa mahujaji yazama Thailand

Ramani ya eneo la ajali Thailand
Image caption Ramani ya eneo la ajali Thailand

Boti moja imezama baada ya kugonga daraja katikati mwa mji wa Thailand wa Ayutthaya,na kuwaua takriban watu saba akiwemo mtoto mmoja kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Boti hilo lilikuwa likisafiri kupitia mto Chao Phraya wakati ajali hiyo ilipotokea.

Lilidaiwa kuwabeba zaidi ya watu 100 na huenda idadi ya waliofariki na wale waliotoweka ikaongezeka.

Ajali hiyo ilitokea karibu na hekalu la Wat Sanam Chai ,ambalo ni maarufu sana na watalii.

Abiria walikuwa wakisafiri kutoka Nonthaburi ,makaazi ya mji mkuu Bangkok kuelekea Ayutthaya kwa ibada ya dini ya Kiislamu kulingana na gazeti la the Bangkok Post.