Chama cha Merkel chapoteza viti uchaguzi wa majimbo

Angela Merkel Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Angela Merkel

Chama cha Christian Democrats cha Kansela Angela Merkel kimeripotiwa kupoteza viti vingi katika mji wa Berlin, kufuatia kura zilizopigwa kwenye uchaguzi wa majimbo nchini Ujerumani.

Chama cha Mrengo wa kulia kinachopinga wahamiaji -AFD-, kinaonekana kupata nguvu na kinajipanga kushinda viti bungeni kwa mara ya kwanza.

Umaarufu wa Angela Merkel umepungua kufuatia sera yake ya kuwaruhusu wakimbizi kuingia nchini humo.

Chama cha AFD sasa kitawakilisha majimbo 10 kati ya kumi na sita bungeni.

Mwandishi wa BBC mjini Berlin anasema chama cha Angela Merkel kwa kiasi kikubwa kinaweza kuondolewa katika serikali ya muungano ya Berlin na chama cha mrengo wa kushoto cha Social Democrats ambacho kinaonekana kupata nguvu kubwa.