Chama tawala cha Putin Urusi chaongoza uchaguzi wa bunge

Rais Vladmir Putin Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Vladmir Putin

Chama cha rais Vladimir Putin wa Urusi, kimepata ushindi mkubwa katika chaguzi za bunge.

Uchaguzi huo unafanyika ikiwa imebaki miaka miwili tu, Rais huyo wa Urusi, kutafuta awamu ya nne kuiongoza nchi hiyo.

Tume ya uchaguzi imesema kuwa kwa robo ya kura zilizohesabiwa, chama cha United Russia imeshinda kwa zaidi ya asilimia hamsini.

Rais Putin amesema kwa sasa nchi inakabiliwa na wakati na hali mgumu, lakini bado wanakiunga mkono chama chake.

Kama ilivyokuwa katika uchafguzi wa mwaka 2011, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilipungua, hususan katika miji mikubwa miwili ya Moscow na Saint Petersburg.

Mmoja wa viongozi wa upinzani Mikhail Kasyanov, amesema hali hii inaonyesha wazi kuwa Warusi wameacha kuamini kwamba kura zinaweza kubadilisha chochote.