Marekani yachunguza kubaini walioshambulia New York

FBI Haki miliki ya picha AP
Image caption FBI wamekanusha madai yaliyoenea awali kwamba washukiwa watano wamekamatwa

Wachunguzi mjini New York wanafuatilia ushahidi kubaini kuhusu ni nani alitega bomu lililolipuka katika wilaya ya Chelsea huko Manhattan siku ya Jumamosi usiku.

Watu wote 29 waliojeruhiwa wameondoka hospitalini.

Shirika la ujasusi la FBI linachunguza kifaa cha pili ambacho hakikulipuka kilichopatikana neo lililo karibu pamoja na bomu lingine lililopuka katika jimbo la New Jersy saa chache kabla.

Usalama umedumishwa kote mjini New York huku maelfu ya maafisa zaidi wa usalama wakitumwa.

Kwingineko, shirika la ujasusi la marekani FBI linachunguza madai ya kundi la Islamic State kuwa mmoja wa wafuasi wake waliendesha shambulizi la kisu katika jimbo la minnesota nchini marekani siku ya Jumamosi.

Mwanamme aliyekuwa amevaa sare za maafisa wa usalama aliwachoma kisu watu 9 kabla ya kuuwa kwa kupigwa risasi na polisi ambaye alikuwa likizo.

Vyombo vya habari vinasema kuwa mtu huyo ni wa asili ya Somalia. Hakuna mtu aliyepata majeraha mabaya kati ya wale waliojeruhiwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii