UNHCR: Nchi za Ulaya ziungane kuwasaidia wakimbizi

Mwanamke atembea karibu na maboya yanayotumiwa na wahamiaji Chios, Ugiriki Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwanamke atembea karibu na maboya yanayotumiwa na wahamiaji Chios, Ugiriki

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi limetoa wito kwa serikali za nchi za Ulaya kuwa mstari wa mbele katika kutatua mzozo kuhusu wakimbizi.

Akizungumza katika siku ambayo Umoja wa Mataifa unaandaa mkutano wake wa kwanza mkuu kuhusu wakimbizi, mkuu wa UNHCR Filippo Grandi ameambia BBC kwamba mataifa binafsi sharti yaungane na kuonyesha ukarimu kwa watu wanaotoroka vita na unyanyasaji.

Amesema ni muhimu pia kuwasikiliza wanaopinga wahamiaji lakini akakosoa wanasiasa wanaowapinga wahamiaji akisema ni makosa kueneza wasiwasi kwa kutumia 'habari za uongo."