Siri ya Mzee Senga na Mzee Pembe kufanikiwa
Huwezi kusikiliza tena

Siri ya Mzee Senga na Mzee Pembe kufanikiwa Tanzania

Sanaa ya uchekeshaji Afrika Mashariki inazidi kukua, ambapo wachekeshaji wanaochipukia wamepata mafanikio makubwa na kuweza kusafiri maeneo mbali mbali Duniani sababu ya vijapi vyao. Lakini ni akina nani walitengeneza msingi huo?

Kwa Tanzania, Ulimboka Mwalulesa almaarufu kama Mzee Senga na Yusufu Kaimu yaani Mzee Pembe ni wachekeshaji waliodumu kwa miaka mingi hadi sasa na bado wanaendelea.

Mwandishi wa BBC Arnold Kayanda amezungumza nao kupata mtazamo wao kuhusiana na fani hii.