Mshambuliaji wa Minnesota ni ''mzaliwa wa Kenya''

Dahir Adan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dahir Adan

Mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio la kisu la kundi la Islamic State huko Minessota nchini Marekani katika duka moja kubwa siku ya Jumapili ametambulika kuwa mzaliwa wa Kenya Dahir Adan.

Kulingana na gazeti la The Star Tribune,babake mshambuliaji huyo alimtaja licha ya kutotambuliwa rasmi.

Watu tisa walijeruhiwa kabla ya mshambuliaji kupigwa risasi na kufariki na afisa wa polisi ambaye hakuwa katika zamu siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Minnesota

Pia ameliambia gazeti hilo kwamba mwanawe wa miaka 22 alizaliwa nchini Kenya lakini akakulia nchini Marekani.

Gazeti hilo limeripoti kwamba Adan alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha St Cloud.