ICC: Kenya ilikataa kushirikiana nasi kikamilifu

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Mahakama ya kushughulikia makosa ya jinai ya ICC, yenye makao yake makuu huko The Hague nchini Uholanzi, imeelezea Kenya na mamlaka kuu nchini humo, kuwa ilishindwa kushirikiana kikamilifu na mahakama hiyo, kuhusu kesi yake ya hivi majuzi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta.

Bwana Kenyatta alikuwa ameshtakiwa katika mahakama hiyo, kwa makosa dhidi ya binadamu, kwa kuhusika kwake katika ghasia zilizotokea nchini Kenya, wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, lakini kesi hiyo baadaye ilitupiliwa mbali.

Wachanganuzi wanasema kwamba matamshi hayo ya sasa, yatatia doa uhusiano kati ya Kenya na mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta, ameliomba bunge la nchi yake, kupitisha sheria ya kujiondoa kwa Kenya, kutoka kwenye mahakama hiyo ya ICC.