Ashtakiwa kwa kutaka kuua polisi Marekani

Haki miliki ya picha NYPD
Image caption Ahmed Khan Rahami

Mhamiaji wa Kiafghan nchini Marekani ambaye ni mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya mwishoni mwa wiki, katika miji ya New York na New Jersey ameshtakiwa kwa makosa matano ya kupanga kuua polisi.

Ahmed Khan Rahami mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa mapema kufuatia ufyatulianaji wa risasi na polisi, hali ambayo pia ilimsababishia majeraha.

Rahami kwa sasa anashikiliwa hospitalini.

Huenda akakabiliwa na mashtaka zaidi yanayohusu mashambulizi ya mabomu.

Meya wa New York Bill de Blasio anasema kuna sababu ya kuamini kuwa mashambulizi hayo ni vitendo vya ugaidi.