British Colonial Co: Mgahawa wenye mfano wa enzi za ukoloni

Haki miliki ya picha BRITISH COLONIAL CO.
Image caption Mgahawa wa British Colonial Co. upo mjini Brisbane

Mgahawa mmoja huko Australia umeshutumiwa kwa kuendekeza ubaguzi wa rangi na ukoloni kutokana na kujengwa na kuendeshwa mithili ya enzi za ukoloni wa Uingereza.

British Colonial Co, uliofunguliwa Julai huko Brisbane, umesema unasherehekea siku na utawala wa ukoloni wa Uingereza.

Mgahawa huo umesema ''umesikitishwa'' na taarifa kwenye vyombo vya habari.

"tunajivunia biadhaa zetu, maandalizi, na mapokezi kwa wateja tuliowavutia," ulisema katika taarifa yake.

"tumesikitishwana taarifa za leo kwenye vyombo vya habari kuwa tunawatusi na kudhalilisha jamii. Hilo halikuwa dhumuni letu."

Haki miliki ya picha FACEBOOK
Image caption Mteja mmoja wa Facebook alikarabati utangulizi wa mgahawa huo

Majibizano katika mtandao wa kijamii wiki hii yameshutumu ujumbe wa mauzo wa mgahawa huo kwa kupuuza athari za utawala wa ufalme wa Uingereza dhidi ya Australia na nchi nyengine.

"Suala ni kuwa walitukuza ukoloni bila a heshima kwa jamii iliyoteseka Australia kutoka na ukoloni huo," amesema mtu mmoja katika ukurasa wa mgahawa huo kwenye Facebook.

Mwingine kwenye Twitter amependekeza mtu atembelee mgahawa huo iwapo yupo Brisbane na anajiskia na "utawala wa kikoloni na mauaji ya kimbari kaa mlo".

Wengine hawakuhisi kwamba jina na mapambo ya mgahawa huo yana tatizo lolote.

" Hakuna makosa kujivunia Ufalme. Uingereza iliwajibika kusaidia kuinua maisha ya watu katika maeneo mengi duniani kuliko nchi nyengine yoyote iliotawala". Amesema mteja mmoja wa Facebook.

Mvutano huu unaonekana kuathiri shughuli katika mgahawa huo.

Na ujumbe wa kunadi mgahawa huo kibiashara umebadilishwa kutoka:

"mgahawa umejengwa kutokana na utawlaa wa kifalme kwa kuendeleza utamaduni wa dunia".

Na sasa unasema: "fursa ya kipekee na ya kisasa ya kupata mlo katika mandhari ya kusisimua kutoka mashariki kuelekea magharibi."